Instagram yamponza Mesut Ozil kwa kocha wake
Nyota wa kimataifa wa Ujerumani anayeitumikia kikosi cha washika mitutu wa London nchini England Mesut Ozil inaonekana kama kitendo cha kocha wake Unai Emery kumuacha katika safari ya kwenda kucheza mchezo wa 32 dhidi ya BATE hakupenda na imebainika hiyo kufuatia kulike comment ya shabiki wake aliyocomment katika post yake ya Instagram.
Unai hadi sasa licha ya kuwadai Mesut Ozil kuwa alikuwa anaumwa kwa siku za karibuni, amempa nafasi ya kucheza dakika102 ndani ya mwaka 2019, hivyo kitu ambacho kimemfanya kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani anayeoongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa Arsenal wa pauni 350000 kutokuwa na furaha.
“Tunakukumbuka sana kaka endelea kupambana, urudi uwe imara na muoneshe Unai, wachambuzi wa ajabu na dunia nzima kwa ujumla kuwa hawakuwa sahihi” comment ya shabiki instagram aliyo-like Ozil iliyozidi kuchochea makaa ya moto katika uhusiano wake na Unai Emery.
Baada ya Unai kuulizwa kwa nini alimuacha Ozil katika safari ya kwenda kucheza na BATE nchini Belarus alijibu hivi “Tuko hapa na wachezaji ambao nafikiri wapo timamu kucheza, wachezaji ambao hawapo kikosini ni kwa sababu hawako sawa Ramsey hakufanya mazoezi na timu, Sokratis ameanza mazoezi ila hayupo sawa kama ilivyo kwa Ozil” alisema Unai Mbele ya waandishi.
Katika mechi hiyo ya kwanza hatua ya 32 bora, Arsenal walipoteza kwa goli 1-0, sasa wanasubiri kucheza mechi ya marudiano Februari 21 katika uwanja wa Emirates, London.