Yanga wapiga dua Morogoro kuelekea mechi ya watani
Kuelekea mchezo wa watani wa Jadi Yanga na Simba,Timu ya Yanga imefanyiwa dua muda mfupi kabla ya kutoka mjini Morogoro.
Yanga wanatarajia kurejea Leo kutoka Morogoro walikokuwa wameweka Kambi ya siku 5 kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Simba utakaochezwa februari 16 mwaka huu ( jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na #Worldsports14 Mratibu wa Klabu hiyo Hafidhi Salehe amesema kuwa wameamua kufanya dua hiyo ili mwenyezi mungu awasaidie waweze kushinda katika mchezo huo.
.
“Tumeamua kumshirikisha Mungu katika hili ili atusaidie tuweze kufanya vizuri katika mchezo wetu dhidi ya Simba na ninaimani tutafanya vizuri” amesema Hafidhi
Watani hao wanakutana kwa mara ya pili katika msimu huu,ikiwa mchezo wa kwanza walitoka Suluhu.
Pia watani hawa wanakutana huku Yanga akiwa amecheza michezo 23 akiwa na point 58 na anashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi kuu huku Simba akiwa amecheza michezo 15 akiwa na point 36 na anashika nafasi ya 4 katika msimamo huo.