Nyoni aanza mazoezi Simba
Mchezaji wa Klabu ya Simba Erasto Nyoni ameanza mazoezi mepesi leo baada ya kukaa nje ya Uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo.
Daktari wa Timu hiyo Dk.Gembe amesema kuwa hali ya Nyoni kwa sasa anaendelea vizuri na leo ameanza mazoezi mepesi.
“Hali ya Mchezaji wetu Nyoni anaendelea vizuri na leo ameanza mazoezi mepesi kidogo kidogo huku tukiendelea kumuangalia” amesema Dk Gembe