Solskjaer amshauri Anthony Martial
Mwalimu wa Manchester United wa mpito Ole Gunnar Solskjaer amemuweka nyota wa timu hiyo Anthony Martial katika level za mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ambaye amewahi kuichezea timu hiyo kwa miaka kadhaa kabla kwenda Real Madrid 2009.
Solskjaer ambaye alikuwa anaongea na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint Germain katika uwanja wa Old Trafford, alieleza Martial ana kipaji kama cha Cristiano Ronaldo hivyo ni kazi kwake kuamua tu kufikia alipo Cristiano Ronaldo na aliyoyafanya Manchester United.
“Kama anataka kuwa katika kiwango cha Cristiano Ronaldo, Anthony Martial anajua nini cha kufanya hiyo ni juu yake kwa sababu ana kipaji” alisema kocha Ole Gunnar Solskaer wakati anaongea na waandishi wa habari.