Rekodi ya Solskjaer yavunjwa Solskjaer
Matumaini makubwa yaliokuwepo kwa mashabiki wa Manchester United dhidi ya Paris Saint Germain katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya imeenda tofauti, baada ya PSG kuharibu shughuli wakiwa Old Trafford.
Wadau na mashabiki wa soka katika mchezo huo walikuwa wanaamini wa Manchester United atapata matokeo chanya dhidi ya PSG, tena ikiwezekana kwa ushindi wa mabao mengi zaidi, hiyo inatokana na kucheza nyumbani na PSG kuwakosa nyota wake muhimu.
Manchester United walikuwa wanacheza na PSG ambayo ilikuwa imejikatia tamaa kwa hofu ya kuwakosa nyota wake watatu waliokumbwa na majeruhi Edinson Cavani, Neymar na beki wake Thomas Meuner aliyeumia siku tatu nyuma lakini pia kuwa katika uwanja wao wa nyumbani ingeweza kuwasaidia.
Mambo yamekuwa tofauti na Manchester United kujikuta rekodi ya Ole Gunnar Solskjaer kuingoza Manchester United katika michezo 10 mfululizo pasipo kupoteza mchezo inaishia , baada ya kupigwa Manchester United kwa mabao 2-0 yaliofungwa na Kimpembe dakika ya 53 na Mbappe dakika ya 60, hivyo tarehe 6 Machi mchezo wa marudiano Manchester United anatakiwa kushinda kwa mabao 3-0 na kuendelea au 3-1 ili apate fursa ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo.