Ripoti ya Sala imetolewa rasmi
Baada ya mwili wa mshambuliaji wa Kiargentina aliyekuwa anaichezea Nantes FC ya nchini Ufaransa Emiliano Sala kupatikana ukiwa chini ya bahari kwenye ndege ndogo waliyokuwa wanasafiria Sala na rubani wake David Ibbotson kutokea Nantes kurudi Cardiff City sasa imetolewa ripoti ya uchunguzi.
Mwili huo ulipatikana na kwenda kufanya uchanguzi Maabara kuweza kutambua ni mwili wa nani kati ya Emiliano Sala na rubani wake, kwani mwili huo ulikuwa umeharibika vibaya kutokana kukaa chini ya maji kwa zaidi ya wiki, baada ya uchunguzi mwili huo ulibainika ni wa Emiliano Sala na mwili wa rubani wake haujaonekana mpaka leo.
Ripoti kamili ya jopo la madaktari imetoka baada ya kuuchunguza mwili wa Emiliano Sala, jopo la madaktari wanaeleza kuwa Emiliano Sala baada ya ajali kutokea alipoteza maisha baada ya kuumia sana sehemu za kichwani na kifuani, kiasi kilichopelekea mwili wake kutambuliwa kwa kupima alama za vidole (Fingerprint)
Tukukumbushe Emiliano Sala akiwa katoka kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Cardiff City ya Wales akitokea Nantes kwa rekodi ya usajili wa klabu hiyo, alipata ajali akiwa katika ndege ndogo Piper Malibu pamoja rubani wake David Ibbotson ambaye mwili wake haujaonekana hadi leo toka January, hiyo ni baada ya Sala kutaka kurudi Cardiff baada ya kumaliza kuwaaga wachezaji wenzake wa Nantes.