Aaron Ramsey huyooo Juventus
Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey ameripotiwa kusaini mkataba wa awali na Juventus ya Italia ambao atajiunga nao rasmi katika majira ya kiangazi mwaka huu kwa mkataba wa miaka minne.
Ramsey,28, atakuwa anapokea mshahara wa pauni 400,000 (Tsh Bilioni 1.1) kwa wiki Juventus na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Uingereza anayelipwa zaidi katika mshahara.