Scholes apata kazi ya ukocha Uingereza
Kiungo wa zamani wa timu ya Manchester United Paul Scholes leo Februari 11 ametambulishwa rasmi kama Kocha mpya wa timu ya Oldham Athletic ya Ligi daraja la pili nchini Englans (Ligue 2)
Scholes mwenye umri wa miaka 44 kwa sasa moja katiya changamoto atakayokutana nayo akiwania kupandisha timu hiyo, kutoruhusiwa kusajili au kuuza mchezaji kutokea Salford City kwenda Oldham au kutoka Oldham kwenda Salford City.
Maamuzi hayo ambayo yatajadiliwa na bodi ya EFL hivikaribuni, inaelezwa kuwa vitawekwa vizuizi hivyo kwasababu inafahamika kuwa Scholes ana hisa ya asilimia 10 katika umiliki wa timu ya Salford City hivyo mwamuzi yoyote yatakayokuwa yanahusisha klabu mbili hizo yatakuwa ya mgongano wa kimaslahi kwa Scholes.