Sarri asema sababu ya kutompa mkono Guardiola
6-0 ndio kipigo alichopata Chelsea kutoka kwa Manchester City jana katika uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa ligi kuu nchini England.
Baada ya mchezo huo kocha wa Chelsea Maurizio Sarri alionekana kukataa kumpa mkono kocha wa Man City Pep Guardiola kama ilivyo kawaida mechi inapomalizika.
Wakati anahojiwa na Sky Sports baada ya mechi Pep Guardiola alisema kuwa aliongea na kocha msaidizi wa Chelsea Gianfranco Zola na kumwambia kuwa Sarri hakumuona.
.
“ Niliongea na Gianfranco Zola . (Sarri) Hakuniona mimi, “ Alisema Pep.
Sarri akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi alisema “ Sikumuona kwa muda ule lakini nitaenda kumsalimia baadae, kama kawaida .”