Gareth Bale aweka rekodi yake Real Madrid
Gareth Bale akitokea benchi jana ameisadia Real Madrid kuondoka na ushindi dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid akifunga goli moja kwenye ushindi wa 3-1 wa ugenini katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania.
Goli hilo linamfanya Gareth Bale kuwa amefunga jumla magoli 100 katika klabu ya Real Madrid, huku ushindi huo ukiwapeleka mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa LaLiga huku Atletico Madrid chini ya kocha wao Diego Simeone wakishushwa kutokana nafasi ya pili mpaka ya tatu.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Atletico Madrid kumaliza mechi wakiwa 10 kufuatia kiungo wao Thomas Partey kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya njano ya pili, magoli yaliwekwa wavuni na Casemiro, Sergio Ramos kwa penati na Gareth Bale akifunga goli la mwisho , huku Antoine Griezmann akifunga bao pekee la Atletico Madrid.