Bank sasa yupo huru kucheza ligi kuu
Leseni ya kiungo wa Klabu ya Yanga Mohamed Issa Juma ‘Banka’ tayari imetumwa Yanga na Shirikisho la soka nchini ( TFF), hii ina maana kuwa Banka yuko huru kucheza mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania endapo benchi la ufundi wataona inafaa kumtumia kulingana na mazoezi aliyoyafanya. Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizo ruhusiwa michezoni ya kanda ya tano Afrika RADO octoba 31 mwaka 2018 ilimfungia Banka kuto jihusisha na masuala ya Soka kwa kosa la matumizi ya dawa zisizo faa michezoni.
Banka alikutwa na hatia hiyo akiwa nchini Kenya kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup na kikosi chake ya timu yake ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’