Mendy asema ukweli asigombane na Guardiola
Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester City ya nchini England Benjamin Mendy ambaye sasa hivi anauguza majeraha yake, ameonekana kuleta utata katika mitandao ya kijamii baada ya post yake aliyopost insta story na kuandika kuwa yupo Hong Kong wakati siku mojanyuma alisema yupo Barcelona.
Baada ya kuonekana akiwa sehemu tofauti tofauti waandishi wa habari walimuuliza kocha wa mchezaji huyo kuhusiana na wapi alipo mchezaji huyo ndipo Pep Guardiola aliposhangaa na kueleza kuwa yeye anafahamu Benjamin Mendy alimuaga anakwendaUfaransa kwa siku moja na sio Hong Kong.
“Alisema anaenda Paris (Ufaransa) lakini Hong Kong nimbali sana nafikiri nahitaji kupakuwa app ya instagram ili niwe na account, kiukweli itakuwa sio sawa kamakweli atakuwa Hong Kong” alisema Pep Guardiolawakati anahojiwa na waandishi wa habari.
Baada ya muda kupita na stori hiyo kusambaamitandaoni Benjamin Mendy aliamua kueleza kuwa amedanganya eneo alilokuwepo alikuwa akifanya masikhara na dereva wake wa uber kuwa hataki matatizona Pep “Ulikuwa ni utani kati yangu na dereva wangu waUber, sitaki matatizo na Pep”