Yanga wasema mapambano ya Ubingwa bado ni makali
Baada ya kutoka sare ya kutokufungana dhidi ya Singida United Kaimu mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Samuel Lukumay amesema kuwa mapambano ya Ligi kuu bado ni makali kwa Timu zote zinazoshiriki Ligi hiyo kutokana na mechi zinavyochezwa na matokeo wanayoyapata.
“Matokeo ya jana hayakuwa mazuri kwetu tunajipanga tena kwa mchezo wetu unaofuata dhidi ya JKT na mapambano bado ni makali ya kuweza kujua nani atakuwa Bingwa wa Ligi kuu Msimu huu” amesema Lukumay
Pia kikosi cha Yanga kimeanza safari ya kurejea jijini Tanga kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa februari 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ikumbukwe kuwa Februari 3 Yanga Alikutana na Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga na kwenda mkoani Singida februari 4 na kucheza jana na Singida United na kutoka sare ya bila kufungana.