Hiki ndicho alichopanga kufanya Kompany katika jiji la Manchester
Nahodha wa klabu ya Manchester City ya nchiniUingereza Vincent Kompany ameamua kutokuwamchoyo wa fadhila baada ya kukiri hadharani kuwaamekuwa na wakati mzuri katika maisha yake ya sokakwa muongo (miaka 10) wote mmoja aliyocheza sokalake katika jiji la Manchester.
Nyota huyo wa Manchester City na timu ya taifa yaUbelgiji amekuwa na wakati mzuri toka amejiunga naklabu hiyo mwaka 2008 akitokea klabu ya HumbergerSV ya nchini Ujerumani hadi leo hii na sasa ameamuakuandaa kitu maalum kwa ajili ya kusaini watu wasio namakazi katika jiji la Manchester kama sehemu yakurudisha shukrani kwa jamii.
Kompany ameripotiwa kuwa ameanzisha kampenimaalum itakayoitwa “Tackle Rough Sleeping In The City” Kompany ameweka wazi kuhusu mradi wake huo wa kuhakikisha anasaidia watu wote wanaolalamitaani katika jiji la Manchester kama sehemu yakushukuru kwa mapenzi na sapoti ambayoamekuwa akiipata.
“Nimepokea vingi kutoka Manchester katikamaisha yangu ya soka na nimecheza katikakiwango cha juu na nimekuwa nikiungwa mkonokwa kiwango cha juu kwa wakati wote ambaonimekuwa nikicheza hapa iwe kipindi cha furaha au huzuni, katika kipindi cha miaka 10 nimekuwa nawakati mzuri kuichezea Manchester na kukuzabrand ya timu” alisema Vincent Kompany