Ferguson atoa sababu za kushindwa kumleta Maldini Old Trafford
Wengi wanatamani kujua ni nini kilitokea pale ambapo kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alipojaribu kutaka kumsajili legend wa AC Milan Paulo Maldini, basi jibu limepatikana na kila kitu kimewekwa wazi kupitia mitandao mbalimbali barani Ulaya.
Ferguson ambaye ana umri wa miaka 77 kwa sasa wakati anaifundisha Manchester United alibahatika kusajili wachezaji mbalimbali nyota katika mikono yake lakini Paulo Maldini alichemka kupata saini yake kutokana na baba wa mchezaji huyo Cesare Maldini kukataa kabisa mwanae kwenda Manchester. .
“Nilijaribu kumsajili Paulo Maldini kuja Manchester United lakini nilipokwenda kuzungumza na baba yake (Cesare) alijibu Hapana na akatoa jibu ambalo lilinifanya nitikise kichwa alisema kuwa babu yake yeye ni shabiki wa AC Milan, baba yake ni shabiki wa AC Milan, yeye ni shabiki wa AC Milan na mwanae pia ni AC Milan hivyo sahau kuhusu kumsajili” alisema Sir Ferguson.
Paulo Maldini ambaye ana umri wa miaka 50 kwa sasa aliichezea timu moja tu ya AC Milan katika maisha yake ya soka ambapo alianzia katika timu za vijana (1978-1985) lakini akajiunga na timu ya wakubwa 1985 hadi 2009 na kwa sasa ndio kurugenzi wa michezo wa klabu ya AC Milan, Maldini amecheza jumla ya michezo 647 na kufunga mabao 29.