Nantes yadai pesa za usajili wa Sala kwa Cardiff City
Jopo la wanasheria wa timu ya Nantes FC ya nchini Ufaransa wamekaa chini na kuandaa mpango wa kudai pesa zao za usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wao Emiliano Sala kujiunga na klabu ya Cardiff City ya nchini Wales, Nantes wanataka walipwe malipo yao ya awali ya mchezaji huyo.
Nantes walimuuza Emiliano Sala nyota mwenye asili yaArgentina kwenda Cardiff City kwa uhamisho unaotajwa kuwa wa thamani ya pauni milioni 15 ila mchezaji huyo baada ya kusaini wakati ameenda kuwaaga wachezaji wenzaks Nantes kwa ndege binafsi ila wakati anarudi Januari 21 ndege yao ndogo ilipotea akiwa narubani wake David Ibbston.
Nyota huyo aliripotiwa kuwa ndege yao ilianguka katika bahari na wanahofiwa kufariki, mwili wa mmoja ndio umeonekana na bado haujagundulika n wa nani kati ya Emiliano Sala au rubani wake, Cardiff wanasema hawawezi kuwalipa Nantes FC pesa hizo hadi uchunguzi wa mahali alipo mchezaji huyo ukamilike ambapo wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha na rubani wake.