Barca kuvaa jezi za kusheherekea sikukuu ya China
Usije kupata mshangao katika mechi ya El Clasico ya nusu fainali Copa del rey leo pale utakapoona majina ya wachezaji wa Barcelona yameandikwa kwa lugha ya kichina.
Wachezaji wa Barcelona leo katika jezi zao zitaandikwa tafsiri ya majina yao kwa kwa lugha ya kichina, hii ikiwa ni kusheherekea mwaka mpya wa China.
China kila mwaka husherekea mwaka wao mpya kati ya Tarehe 21 Januari na Februari 20, na mwaka huu wamesheherekea mwaka mpya wao Februari 5.
Barcelona wanafanya hivyo ili kuendelea kukuza wigo wa mashabiki kutoka mashariki ya mbali , hasahasa China.