Guardiola azirudisha Chelsea na Man United katika mbio Ubingwa
Baada ya timu ya Liverpool kupoteza alama nne katika michezo miwili mfululizo ya hivi karibuni ya Ligi Kuu ya nchini England, timu ya Manchester City ilirudishwa katika mbio za kutetea taji lao la Ligi Kuu nchini England ambapo hapo katikati kutokana na kiwango kizuri ilichokuwa imekionesha Liverpool ilipewa nafasi ya kutwaa taji hilo.
Kutokana na Liverpool kupishana na Manchester City kwa alama tatu, baada ya kutoka sare michezo miwili mfululizo Manchester City wakiwa na alama 59 nafasi ya pili na Liverpool nafasi ya kwanza kwa kuwa na alama 62, kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema timu zote sita za juu bado zipo katika mbio na nafasi ya kutwaa taji hilo muachana wa alama ni mchache sana.
.
“Sijasema kwamba Tottenham hawapo katika nafasi ya kuwania Ubingwa au Chelsea, sijaziondoa timu zote tano au sita za juu katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu , wapo wanapambania nafasi hiyo kama Chelsea wanaweza kushinda mechi mfululizo wanaweza kuingia katika mbio hizo, kila timu ina nafasi muachana wa alama sio mkubwa, siku tatu au nne zilizopita tulikuwa tayari tumeondolewa katika nafasi ya kuwania taji hilo nafasi alikuwa kapewa Liverpool lakini kwa sasa tumerudishwa katika mbio hizo” alisema Pep Guardiola
Hata hivyo kauli ya Pep Guardiola inakuja kutokana na timu hizo sita za juu kwa mahesabu na utofauti wa alama zinaweza kuingia katika mbio hizo, kutokana na Ligi bado imebaki na michezo 13 ambapo kama timu inashinda michezo yote iliyobaki wanavuna jumla ya alama 39 ambazo zinaweza kuiwezesha timu kuwa Bingwa wa Ligi hiyo hata kama upo nafasi ya sita, kwa sasa kila timu imecheza jumla ya michezo 25.