Hazard azidi kuwapa Presha Hazard
Nyota wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard bado anaendelea kuacha maswali yasiyokuwa na majibu kwa mashabiki kama ataendelea kuichezea Chelsea au ataondoka mwisho wa msimu, hiyo ni baada ya kuripotiwa kuwa nyota huyo amekiri tayari kufanya maamuzi.
Hazard ameripotiwa kuwa tayari amefanya maamuzi juu ya hatma yake atacheza klabu gani msimu ujao licha ya kuwa hajataja rasmi, kama hufahamu tu Hazard anamaliza mkataba wake na Chelsea unaisha Juni 2020 na anawindwa sana na timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
Hata hivyo Hazard ambaye bado hajakubaliana maslahi binafsi na Chelsea kuhusiana kuongeza mkataba mpya, anaweza akasaini mkataba mpya kama hatopata ofa ya kumridhisha kutoka Real Madrid ambao inadaiwa anawasililizia wao tu .
Nyota huyo ambaye ameichezea Chelsea ya nchini England kwa miaka 7 toka atoke timu ya Lille ya nchini Ufaransa mwaka 2012 akiongea na radio ya RMC ya nchini Ufaransa amenukuliwa akisema kuwa “ Ninajua nitakachofanya, tayari nimeshafanya maamuzi.”