Usiempenda kaja, Messi yupo fiti kuwavaa Madrid
Baada ya nchini Hispania na duniani kote hofu kutanda kuwa mchezo wa nusu fainali wa Copa Del Rey wa Barcelona dhidi ya wapinzani wao Real Madrid leo unaweza kuchezwa bila uwepo wa nyota wao Lionel Messi ambayo alihofiwa kuwa angeukosa mchezo huo kwa majeruhi, mambo yamekuwa tofauti.
Lionel Messi ambaye ni mchezaji tegemeo wa timu hiyo ya FC Barcelona na nahodha pia, sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona kitakachocheza mchezo wa El Clasico leo baada ya kuthibitika tatizo la nyama za paja alilolipata katika mchezo dhidi ya Valencia limetibika.
Tukukumbushe tu Lionel Messia aliumia nyama za paja (thigh injury) wakati wa mchezo wa FC Barcelona wa Ligi Kuu ya nchini Hispania maarufu kama LaLiga dhidi ya Valencia jumamosi iliyopita mchezo ambao ulimalizika kwa kufungana mabao 2-2, Lionel Messi akipachika mabao yote mawili ya Barcelona kwa penati na goli la kawaida.