Liverpool watoa matumaini ya Ubingwa kwa City
Mara nyingi kumekuwa na hulka ya watu mbalimbali kusema kuwa Ligi Kuu ya nchini England ndio Ligi pekee duniani ambaye Bingwa wake hawezi kujulikana hadi dakika za mwisho au mechi tatu au mbili za mwisho, hiyo tofauti na baadhi ya Ligi ambapo imekuwa ikifika mwezi Desemba tu unajua timu ipi itakuwa Bingwa.
Kuonesha hilo ni kweli kuwa Ligi Kuu ya nchini England ina ushindani na timu imara, klabu ya West Ham United imedhihirisha baada ya kuwabana Liverpool wakiwa katika jiji la London na kushindwa kutoka na alama tatu tofauti na wengi walivyokuwa wanadhani, pamoja na kuwa Liverpool wanaongoza Ligi na West Ham kushika nafasi ya 12 hiyo haikuwa ruhusu wao kuondoka na alama tatu na hatimae kulazimishwa sare ya 1-1.
Liverpool ambayo ilitawala mchezo kwa asilimia 74 ilianza kupata bao mapema zaidi ya wenyeji wao West Ham dakika ya 22 kupitia kwa msenegal Sadio Mane lakini haikutosha kuwahakikishia ushindi na kujikuta dakika ya 28 West Ham wanasawazisha kupitia kwa Antonio na kuufanya mchezo umalizike kwa 1-1, sare hiyo ya pili mfululizo kwa Liverpool imeleta matumaini kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Manchester City kuwa wanaweza kutetea taji lao kwa wapo nafasi ya pili wakitofautiana alama tatu tu na Liverpool wanaongoza Ligi kwa kuwa alama 62.