Yanga SC hawalazi damu
Kikosi cha Yanga SC kimeondoka leo jijini Tanga kikielekea Mkoani Singida kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu utakaochezwa Februari 6 dhidi ya Singida United katika uwanja wa Namfua.
Kaimu mwenyekiti wa Klabu hiyo Samweli Lukumay amesema kuwa japo matokeo ya sare ya jana yamewaumiza ila hawakati tamaa na watahakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Singida United.
.
“Timu imefika Arusha hivi sasa na kuelekea Singida kwaajili ya mchezo wetu wa jumatano dhidi ya Singida United, tunaamini tutafanya vizuri katika mchezo huo na niwaombe mashabiki wetu wazidi kutuunga mkono” amesema Lukumay
Yanga bado inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi kwa kuwa na point 54 akiwa amecheza mechi 21 huku Azam akishika nafasi ya pili kwa kuwa na point 47 akiwa amecheza mechi 20.