Mastaa wawili wa Lipuli kuikosa Yanga
Kuelekea mchezo wa kesho kati ya Yanga na Lipuli FC , wachezaji Ally Sonso na Jamali Mnyate hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho utakaochezwa saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa.
Mastaa hao ambao Jamali Mnyate kabla ya kujiunga na Lipuli FC aliichezea Azam pamoja na Simba na Sonso ambaye amejizoelea ustaa akitoka kikosi hicho na kuitwa kwenye Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Afisa habari wa Klabu hiyo Clement Sanga amesema kuwa Mnyate ataikosa mechi ya Yanga ambayo itachezwa kesho Jumanne kwa sababu ya matatizo ya kifamilia wakati Sonso atakosa mechi hiyo kwa kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi iliyopita dhidi ya Mbao FC.
Kwa upande wa maandalizi kuelekea mchezo huo Sanga amesema kuwa toka juzi walipofika Jijini hapa wamefanya mazoezi yakutosha katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
“Maandalizi yapo vizuri timu imekuwa ikofanya mazoezi katika Uwanja wa Chazi, Molali ya Timu ipo juu wachezaji wetu wanaelewa na wanajua nini cha kufanya hapo kesho na ikumbukwe kuwa Yanga anapokutana na Lipuli mechi huwa inakuwa ngumu si Ugenini wala Nyumbani hivyo mchezo wa kesho utakuwa mgumu na tunakwenda kwa tahadhari kubwa sana” amesema Sanga