Pep Guardiola awapa makavu Real Madrid
Kocha wa Man City Pep Guardiola amewaonya Real Madrid kuwa watakutana na ugumu mkubwa kama wanataka kumuondoa kocha Maurcio Pochettino katika klabu Tottenham.
Meneja huyo wa Spurs amekuwa akihusishwa kutakwa na Real Madrid na anaongoza katika orodha ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui Real Madrid.
Licha ya Pochettino kuonekana kukaa mbali na kibarua hicho, Rais wa Real Madrid Fiorentina Perez ameripotiwa kuwa anataraji kujaribu kutuma maombi ya kumchukua kabla ya msimu huu kuisha.
Guardiola anaamini Spurs wanatakiwa kujua kocha wao anahitajika, lakini amesisitiza mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy hatadanganyika kumuachia Meneja wake.
“ Ninafikiri ni kocha mkubwa tayari “ amesema kocha huyo wa Man City.
“ Kwa miaka mingi sasa anafanya mazoezi katika kiwango cha juu zaidi “
“ Alifanya kazi kubwa Espanyol na Southampton, na zaidi hapa Tottenham. Ninaheshimu kazi yake kubwa aliyoifanya katika Career yake na kiuhalisia ni tayari meneja mzuri, hakuna wasiwasi “
“ Amekuwa akihusishwa mara nyingi na Real Madrid. Anaweza kujibu swali hilo – Lakini sijui ni nini kinatokea. Ninachowaza ni Mr Levy si mtu rahisi kufanya nae makubaliano. “
Kocha Julen Lopetegui yupo kwenye Presha kubwa sasa baada ya kipigo cha jana cha 5-1 kutoka kwa Barcelona, huku akiwa nafasi ya 9 katika msimamo wa La Liga wakiwa na Pointi 14.