Hamilton kusepa na ubingwa 5 Formula 1
Simba ikimpiga mtu goli 5, Barca wakishudha kipigo cha goli 5 katia El Clasico , Ni Lewis Hamilton nae anasepa na ubingwa wa Formular 1 kwa mara ya 5.
Dereva wa Mercedes Muingereza Lewis Hamilton amemaliza nafasi ya nne katika mbio za Mexico Grand Prix na kufanikiws kuchukua ubingwa wa Formular 1 mwaka 2018.
Katika mbio hizo za Mexico, dereva wa Red Bull Maxi Verstappen ndiye aliyeibuka mshindi, mpinzani wa Hamilton Sebastian Vettel wa Ferrari akishika nafasi ya pili na Kimi Raikkonen pia kutoka Ferrari akiwa wa 3.
Zikiwa zimebaki mbio mbili msimu kuisha,Brazil na Abu Dhabi, Hamilton anaongoza msimamo wa Madereva akiwa na pointi 358, akimpita mpinzani wake Vettel kwa pointi 64.
Vettel anashika nafasi ya pili akiwa na pointi 294.