Ajibu na Tshishimbi waanza mazoezi mepesi
Wachezaji wa Klabu ya Yanga waliokuwa Majeraha Ibrahim Ajibu pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi wameanza mazoezi mepesi leo kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.
Baada ya mchezo wa Octoba 25 mwaka huu (Alhamisi) uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya KMC na kuibuka na ushindi wa goli 1-0 timu hiyo ilipumzika kwa siku mbili Ijumaa na umamosi Tiku hiyo imeanza mazoezi leo.
Akizungumza na Wordsports14 Msemaji msaidizi wa Klabu ya Yanga Godlisten Anderson Chicharito amesema kuwa hali za wachezaji ni nzuri na wachezaji wao Ajibu na Tshishimbi ambao walikuwa ni majeruhi wameanza mazoezi mepesi baada ya hali zao kuimalika.
“Baada ya mapumziko yetu ya siku mbili timu itafanya mazoezi leo kwenye Uwanja wa Polisi na moja kwa moja imeingia Kambini kwenye Hotel ya Nefaland tayari kwa maandalizi ya mechi yetu ya Jumanne dhidi ya Lipuli Fc itakayochezwa saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa” amesema Chicharito
Chicharito ameongeza kuwa kuhusu kuwatumia wachezaji Ajibu na Tshishimbi ni baada ya kufanya mazoezi yao ndipo mwalimu ataamua kuwatumia au kutowatumia.
Yanga anakutana na Lipuli FC akishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara akiwa na point 22 huku Lipuli FC akishika nafasi ya 13 kwa kuwa na point 12.