KIPIGO KUTOKA YANGA AMRI SAID AMTUPIA LAWAMA GOLIKIPA WAKE
Kocha Mkuu wa timu ya Biashara United inayotokea mkoani Mara Musoma Amri Said amewashushia lawama wachezaji wake baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la FA dhidi ya Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika wakiwa sare ya 2-2.
Amri Said amewatolea lawama hizo wachezaji wake kutokana na kutokuwa makini kwa sababu ya kushindwa kuzuia licha ya kupata nafasi ya kuwa mbele dhidi ya Yanga mara mbili mfululizo, Biashara walipata goli dakika za mapema lakini Yanga wakachomoa na baadae kuongeza tena Biashara ila nidhamu ya ulinzi ikaigharimu timu hiyo.
Kabla ya mchezo kumalizika na makosa kuona mengi kwa mujibu wa Amri Said alifanya mabadiliko ya kumtoa mlinda mlango wake Nurdin Balola na kumuingiza Hassan Robert mabadiliko ambayo hakuyapenda Balola na kujikuta wakizozana na kocha wake Amri Said, kocha wa Biashara anaamini wanatakiwa kujilaumu wenyewe kwani mchezo huo hawakutakiwa kwenda hatua ya matuta.
“Tukirudi tukajilaumu kwa sababu mechi ilikuwa ipo ngumu lakini kwa upande wangu nilijiandaa vizuri ikawa rahisi kiufundi niliweza kumiliki vizuri wachezaji wangu walikuwa wanaweza kuonekana wako timamu lakini mimi nasema tunajilaumu kwa sababu, tumeona kiwango hakikuwa kizuri cha golikipa wangu lakini kiwango pia sehemu ya ulinzi kilikuwa 50/50 mimi nasema mechi ya leo tumeipoteza kwa sababu hatukuwa na umakini zaidi” alisema Kocha Amri Said akihojiwa na Azam TV