Walusimbi atemwa Kaizer Chiefs
Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini jana ikiwa siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili nchini humo, limetangaza kuachana na beki wa kimataifa wa Uganda Godfrey Walusimbi akiwa kadumu na timu hiyo kwa miezi kadhaa akitokea Gor Mahia ya Kenya.
Kaizer Chiefs jana imetangaza kuwasajili wachezaji wawili na kumuacha Godfrey Walusimbi, wachezaji waliosajiliwa na Kaizer Chiefs jana ni mlinda mlango Daniel Akpeyi kutokea Chippa United kwa mkataba wa miezi 17 beki wa Bidvest Wits Reeve Frosler akisaini mkataba wa miaka mitatu
Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya klabu hiyo imeeleza kuwa wameamua kumuacha Godfrey Walusimbi kwa sababu klabu yao imevuka idadi ya wachezaji wa kigeni inaotakiwa kuwa nao, hivyo imemuacha ili kukidhi idadi sahihi inayotakiwa, tukukumbushe tu Godfrey Walusimbi alijiunga na Kaizer Chief Agost 22 2018 akitokea Gor Mahia ya Kenya kwa mkataba wa miaka mitatu uliyokuwa unatarajiwa kumalizika 2021.
Kaizer Chiefs wamesema kuwa beki huyo amefanya chaguo la kurudi kucheza nyumbani kwao Uganda.