Kichuya awafuata Himid Mao na Zayd ligi kuu ya Misri
Mchezaji wa kitanzania Shiza Ramadhan Kichuya tayari bahati imemuangukia na kuihama klabu yake yawekundu wa Msimbazi Simba, Kichuya ambaye alisafirikama sehemu ya wachezaji 20 wa Simba waliokwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa tatu wa KundiD klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly sio mali yaSimba tena.
Kichuya baada ya kutua Misri ili awahi dirisha la usajilila nchini Misri ambalo lilikuwa linafungwa leo, amefanikiwa kusaini mkataba na klabu ya Pharco FC yanchini Misri inayoshiriki Ligi daraja la pili na kutolewakwa mkopo katika klabu ya Ligi Kuu nchini Misriinayojulikana kwa jina la ENPPI.
Baada ya mkataba huo Kichuya sasa anakuwa mtanzaniawa tatu kucheza Ligi Kuu ya nchini Misri msimu huubaada ya Himid Mao anayechezea Petrojet na Yahaya Zayd aliyejiunga na Ismaily SC wakitokea Azam FC kwenda kuanza maisha mapya, hiyo ni habari yenye afyakwa soka la Tanzania kwa ujumla.
Hata hivyo timu aliyojiunga nayo Kichuya ipo nafasi ya14 katika Ligi Kuu yenye timu 18 wakiwa na alama 21, Ismaily ya Zayd ikiwa nafasi ya 11 kwa kuwa na alama23 na viporo vine wakati timu ya Himid Mao ya Petrojetikiwa nafasi ya mwisho kwa kuwa na alama 15, timu yaENPPI FC imeanzishwa mwaka 1985 wakati Pharco FC imeanzishwa 2010.