Meneja wa Simba sasa yupo huru
Klabu ya Simba SC ikiwa tayari Alexandria Misri kwaajili ya mchezo wa tatu wa hatua ya Makundi michuanoya klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, jana zimetoka taarifa ikiwa imepita miezi kadhaa toka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kumfungia meneja waoRobert Richard.
Taarifa zilizotoka leo kutoka kamati ya rufaa ya maadiliya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ni kuwandugu Robert Richard ambaye akiwa kama meneja waSimba, alifungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka nafaini ya Tsh Milioni 5 kwa kutuhumiwa kuhusikakuwachelewesha kuwasili kambini kwa wakati wachezajiwa Simba waliokuwa wameitwa katika kikosi cha timuya taifa ya Tanzania.
Kamati ya rufaa ya TFF jana imetangaza rasmi kufutaadhabu hiyo na ndugu Robert Richard anaruhusiwa kamakawaida kuendelea na majukumu yake, tukukumbusheRobert Richard alifungiwa kujihusisha na soka Septemba11 2018 ikiwa ni miezi minne imepita na siku 20 tokaadhabu hiyo itolewe kwa tuhuma za kuhujumu timu yataifa ya Tanzania kwa kuwa sehemu yawaliowachelewesha wachezaji kuripoti kambini