Timbe afanyiwa upasuaji
Kiungo wa timu ya taifa ya Kenya Ayub Timbe huenda akakosa kipute cha mataifa barani itakayo andaliwa Misri mwezi Juni baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Timbe anatarajiwa kuwa nje kwa kipindi cha miezi mitatu akiuguza jeraha hilo na huenda asiwe tayari kucheza kwenye kipute hicho.
Atokosa mechi ha kufuzu didhi ya Ghana mwezi Machi lakini kukosekana kwake si pigo kwani Kenya ishafuzu katika dimba hilo.
Timbe ana imani kuwa atarejea ugani hivi karibuni.
“Upasuaji umekuwa mzuri na namashukuru mungu. Nina imani kuwa nitarejea kucheza tena hizi karibuni,” alisema kiungo huyo anaye ichezea team ya Beijing Renhe nchini China.
Kenya itarejea kwenye kipute hicho baada ya miaka kumi na tano