Helicopter ya mmiliki wa Leicester City yapata ajali
Helicopter inayomilikiwa na mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha imepata ajali katika viunga vya uwanja wa King Power. Haijafahamika mpaka sasa ni kina nani walikuwapo katika helicopter hiyo.
Polisi wa Leicester wametoa tamko “Tupo tunashughulikia tukio katika viunga vya uwanja wa Kings Power.” Kupitia mtandao wao wa Twitter East Midlands Ambulance Service NHS Trust wameandika kusema kuwa wamepokea taarifa juu ya tukio hili saa 2 na dakika 38 usiku huu na hima walituma daktari, wataalamu wa afya pamoja na Ambulance zilizo na timu kamili ambazo eneo la tukio dakika mbili baada ya kupatiwa taarifa hiyo.
Ripota wa kituo cha SkyNews Rob Dorsett amesema kwenye mida ya saa 2 na nusu usiku, mashuhuda walimueleza kuwa waliona wamiliki wa klabu ya Leicester City wakiondoka katika Helicopter tokea ndani ya uwanja wa King Power kama ilivyo kila wakati katika mechi ila mara hii ilipoteza muelekeo baada ya sekunde chache.
Msemaji wa klabu ya Leicester amesema kwa sasa wanatoa ushirikiano kusaidiana na polisi pamoja na vyombo vingine vya majanga na dharura na watatoa tamko pindi taarifa zote za msingi zitakapo malizika kukusanywa.
Tukio hili limetokea baada ya mechi ya Leicester City dhidi ya West Ham mechi iliyoisha kwa sare ya goli moja kwa moja.
Vichai amekuwa akiondoka uwanjani kwa kutumia Helicopter yake ambayo hupaki katikati ya dimba la King Power katika mechi za nyumbani.
Mthailand huyu na mmiliki wa kampuni ya King Power aliinunua klabu hii mwaka 2010. Katika umiliki wake ubingwa wa ligi ni moja ya mafanikio makuba.
@lcfc
#EPL
#WS14FPL