Neymar awakosa Man United
Nyota wa PSG Neymar atakuwa nje ya uwanja wa kwa muda wa wiki 10 akiuguza mguu wake wa kulia alioumia Januari 23 kwenye mchezo dhidi Strasbourg.
Maumivu hayo sasa yanamkosesha Mbrazil huyo mechi zote mbili za hatua ya 16 bora klabu bingwa Ulaya dhidi ya Man United.
PSG watasafiri kwenda Old Trafford kucheza mechi ya kwanza ya hatua hiyo tarehe 12, Februari na mechi ya marudiano itachezwa Machi 6 jijini Paris.