Niyonzima amkingia kifua Pascal Wawa
Kiungo wa Kinyarwanda anayekipiga na wekundu wa Msimbazi Simba Haruna Niyonzima amelitolea ufafanuzi suala la mchezaji mwenzake raia wa Ivory Coast Pascal Wawa kuwa alitoroka katika kambi ya timu hiyo na kwenda usiku kusherehekea Birthday ya mpenzi wake.
Siku moja kabla ya Simba kucheza mchezo dhidi ya Bandari ya Kenya na kupoteza inadaiwa kuwa wachezaji saba wa Simba walitoroka kambini usiku na kwenda kusikojulikana wakati Wawa ikisambaa video inayohusishwa kuwa ndipo alipokuwa amekwenda kufanya starehe kabla ya mechi.
Simba wakiwa wamewasili Airport Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kuelekea Misri kucheza mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, Haruna niyomzina ameizungumzia video hiyo ya Wawa ambaye ni sehemu ya wachezaji Saba wa Simba waliyodaiwa kutoroka kambini (Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Pascal Wawa, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Mzamiru Yassin)
“Watu wametafsiri tofauti ninaweza kusema hivyo sisi kama wachezaji tunajua hakuna kitu cha hatari kilichotokea, hatujaonekana labda kama video unayo wewe lakini mimi sijaiona, unajua ile video ya Wawa mimi sio kwamba ninamtetea ,ni video ya muda sio ya siku hiyo isipokuwa sisi binadamu tatizo dogo likitokea watu wanaleta na vitu ambavyo vilikuwa havihusiki lakini hayo yamepita sisi tunaangalia mchezo wetu na Al Ahly.”alisema Niyonzima
Klabu ya Simba sasa inaenda kucheza mchezo wake wa tatu wa Kundi D hatua ya Makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kaimu Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Al Ahly waliyomaliza nafasi ya pili katika michuano hiyo msimu uliyopita, Simba wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 3 sasa na AS Vita waliyo nafasi ya pili kwa kuwa na alama 3 ila wamewazidi Simba kwa tofaut ya mbao ya kufungwa huku Al Ahly akiongoza kwa kuwa na alama nne na JS Saoura akishika mkiwa kwa kuwa na alama moja.