Guikan aikimbia Gor Mahia
Mshambulizi wa Ivory Coast Ephrem Guikan ameigura timu ya Gor Mahia na anatarajiwa kujiunga na kilabu ya Buildcon nchini Zambia.
Guikan ambaye aliingia Gor Mahia mwaka wa 2018 hajakuwa akicheza sana kwenye kilabu hiyo na sasa ameondoka baada ya kuafikiana na uongozi wa kilabu.
Mweka hazina wa timu ya Gor Mahia Sally Bolo amethibitisha kuondoka kwa Guikan kutoka Gor Mahia.
“Guikan ameondoka. Aliomba kilabu iweze kumwachilia na tukaafikiana kumpa barua itakayo mwezesha kujiunga na kilabu ingine. Tunamtakia mema katika siku zijazo,” alisema Bolo.
Awali Guikan alikuwa amehusishwa na uhamisho kuelekea Simba ya Tanzania.