Ferguson amkataa Maradona mbele ya Messi
Ukiachana na ubishi wa muda wote ambao haujawahi kupatiwa majibu kati ya wachezaji Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa FC Barcelona nani bora kukosekana majibu, inaaminika nguli wa Argentina Diego Maradona ni bora wa muda wote wa soka kuwahi kutokea akiwekwa level moja na nguli wa Brazil Pele.
Baadhi ya watu pia wamewahi kuhoji wakati Diego Maradona anacheza na Lionel Messi wa sasa nani bora? Wengi walikuwa wakisema Maradona ni bora huku wengine wakifika mbali zaidi na kusema kuwa kumfananisha Messi na Maradona ni kumkosea heshimu mkongwe wa Argentina aliyewahi kutamba na klabu ya Napoli Diego Maradona.
Kocha wa zamani wa Manchester United ambaye ni miongoni mwa makocha wenye heshima kubwa katika mchezo wa soka Sir Alex Ferguson, amewashitua wengi baada ya kuamua kutoa mtazamo wake kwa anachokiamini kuhusiana na Diego Maradona na Lionel Mess, Sir Alex Ferguson ameshindwa kuwa mnafiki na ameweka wazi kuwa kwake yeye Messi huyu ni bora zaidi ya Diego Maradona aliyekuwa katika ubora wake.
“Kwa hilo nitakuwa upande wa Graeme Souness kuwa Messi ni bora zaidi ya Maradona, kwa sababu wakati Maradona anacheza soka alikaa katika kiwago cha juu kwa miaka michache sana ukilinganisha na Lionel Messi” alisema Ferguson
Ferguson ameungana na mchezaji wa zamani wa Liverpool Graeme Souness kuwa Messi ni bora kuliko Maradona na kupingana na kauli ya marehemu rafiki yake Hugh McIlvanney ambaye alikuwa ni muandishi wa michezo aliyekuwa akiamini Maradona ni bora zaidi ya Messi, Hugh McIlvanney alifariki Januari 24 2019 akiwa na umri wa miaka 84.
Tukukumbushe tu Lionel Messi ameshinda mataji 22 mara 4 Ligi ya Mabingwa Ulaya, LaLiga 9, Copa del Rey 6, klabu Bingwa Dunia 3, usindi wa tuzo binafsi Ballod d’Or mara 5 na amecheza jumla ya michezo 128 akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina na kufunga mabao 65 wakati Maradona saba ngazi ya klabu nane pamoja na Kombe la Dunia akiichezea Argentina michezo 91 na kuifungia mabao 34.