Zahera awapa Simba ushauri wasipigwe 5 tena
Klabu ya Simba SC ikiwa na kikosi cha jumla ya wachezaji 20 na viongozi kadhaa leo jioni kitaondoka Dar es Salaam kueleke Misri katika mji wa Alexandria utakapochezwa mchezo wao wa tatu wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly
Simba wanaenda misri wakiwa na kidonda cha kufungwa mabao 5-0 katika mchezo wao wa pili wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita wakiwa mjini Kinshasa nchini Congo DR, kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametoa ushauri ili isijirudie Simba wakafungwa tena tano nyingine.
.
“Kazi ya kocha na wale viongozi kwa asilimia 60 kwa sasa ni kutayarisha wachezaji kiakili na kwa asilimia 40 kiufundi , kwa sababu gani kile kidonda walichofungwa tano bado kipo katika vichwa vya wachezaji inafaa ipone kwenye vichwa vya wachezaji na ili ipone, huwezi kwenda kucheza mechi na Al Ahly halafu useme wewe unabakia tu na mbinu kufungwa tena tano inaweza ikajirudia inabidi wachezaji wapone kwa kuwaambia maneno” alisema Mwinyi Zahera katika mahojiano maalum na Azam TV
Klabu ya Simba sasa inaenda kucheza mchezo wake wa tatu wa Kundi D hatua ya Makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Al Ahly waliomaliza nafasi ya pili katika michuano hiyo msimu uliyopita.
Simba wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 3 sasa na AS Vita waliyo nafasi ya pili kwa kuwa na alama 3 ila wamewazidi Simba kwa tofaut ya mbao ya kufungwa huku Al Ahly akiongoza kwa kuwa na alama nne na JS Saoura akishika mkiwa kwa kuwa na alama moja.