Giroud amkimbia Higuain Darajani
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud amesema anaweza kurejea kucheza nchini kwao Ufaransa baada ya timu yake kumsajili Gonzalo Higuain
Giroud ameifungia the blues goli moja tu katika ligi msimu huu na amekuwa akipata nafasi ndogo ya kucheza.
Chelsea imemsajili Gonzalo Higuain kwa mkopo wa muda mfupi akitokea Juventus. Kabla ya kutua Chelsea Muargentina huyo alikuwa akicheza AC Milan kwa mkopo.