Mnyama kumfuata Mwarabu kesho
Klabu ya Simba inataraji kuondoka nchini Tanzania kesho Januari 29 kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mechi yao ya Klabu Bingwa dhidi ya Al Ahly.
Simba ambayo ina pointi 3 ikishika nafasi ya tatu katika kundi lake ilipoteza mchezo wao uliopita wa michuano hiyo wakicheza na AS Vita nchini Congo na kupokea kipigo cha goli 5-0.
Mechi hiyo ya Simba dhidi ya Al Ahly itapigwa jumamosi hii Februari 2 nchini Misri.