VICTOR MOSES ANAENDELEZA MAISHA YAKE YA MKOPO ATUA UTURUKI
Winga wa Chelsea raia wa Nigeria leo ametangazwa rasmi kutolewa kwa mkopo na klabu hiyo na kwenda kujiunga na timu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki, huo ukiwa ni muendelezo wa kocha wao mpya Maurizio Sarri kuendelea kujenga kikosi chake kwa kuwachukua wachezaji wake wanawahitaji katika mfumo wake.
Pamoja na kuwa Victor Moses ana muda mrefu hayupo Chelsea anacheza katika vilabu vya Liverpool, Stoke City na West Ham United kwa mkopo, Maurizio Sarri kutokana na mchezaji huyo kuwa Chelsea alikuwa na uwezo wa kumrejesha kutoka alipokuwa anacheza kwa mkopo ila kumtoa kwa mkopo wa muda mrefu Fenerbahce inaonesha kutokuwa katika mipango yake.
Moses mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu mwaka mmoja na nusu, toka asajili mwaka 2012 akitokea Wigan Athletic Victor Moses ameshindwa kudumu na Chelsea na kujikuta anatolewa kwa mkopo katika vilabu mbalimbali karibia kila msimu.