KUMBE WACHEZAJI WALIKUWA HAWAMTAKI THIERRY HENRY AS MONACO
Baada ya klabu ya AS Monaco kukumbwa na jinamizi la matokeo mabovu kila kukicha kutokana na kupoteza kila leo kiasi cha kuwa nafasi ya pili kutokea mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini Ufaransa msimu wa 2018/2019, uongozi wao unaonekana kuzidi kutafuta suluhu ya tatizo hilo.
Ikiwa imepita siku moja toka klabu hiyo itangaze kumfukuza kazi kocha wao Thierry Henry aliyedumu na timu hiyo kwa siku 104 toka ajiunge nayo kurithi nafasi ya Leandro Jardim aliyekuwa kafukuzwa, leo klabu imetangaza kumfuta kazi Thierry Henry na kumrejesha kocha wao Leandro Jardim ambaye walimfuta kazi miezi mitatu iliyopita.
Inaelezwa kuwa uongozi wa AS Monaco wamefikia uamuzi wa kumrudisha Leandro Jardim kutokana na wachezaji wao kuwashawishi kuwa wanamuhitaji kocha wao huyo wa zamani hivyo kwa namna yoyote Henry asingekuwa na uwezo wa kufanya vizuri, kwani inaelezwa kulikuwa kuna mgomo baridi ili arudishwe Leandro Jardim , hata hivyo vyanzo vinaeleza nahodha wa AS Monaco alienda kwa uongozi kuwasilisha maombi ya wenzake.
Hivyo uongozi umeona ni busara kufuata matakwa ya wachezaji wao ili kuinusuru na timu yao kushuka daraja, vyanzo vinasema kuwa chanzo Jardim kufanya vibaya hadi wakamfuta kazi hakikutokana na kocha huyo ila uongozi kupuuza baadhi ya mapendekezo yake, Henry anaondoka AS Monaco akiwa kaifundisha katika michezo 20, ameshinda michezo minne, sare 5 na amepoteza michezo 11.