Djokovic uso kwa uso na Nadal Australian Open
Novak Djokovic atacheza mechi ya Rafa Nadal katika fainali ya Australian Open 2019 baada ya kufumnga mfaransa Lucas Pouille 6-0, 6-2, 6-2 katika mchezo wa nusu fainali leo.
Hii itakuwa ni mara ya nane wawili hao kukutana katika fainali ya Grand Slam.
Itakuwa ni fainali ya 7 ya Djokovic katika michuano hii na ya kwanza tangu 2016. Ameshinda fainali zote sita alizocheza kwenye michuano hii.
Mara ya mwisho wawili hao kukutana katika Australian Open ilikuwa mwaka 2012 katika mchezo wa fainali ambao ulichezwa kwa saa tano na dakika 53, Djokovic akiibuka mshindi.