Obi Mikel arejea England
Kiungo wa zamani wa timu ya Chelsea ya nchini England John Obi Mikel hatimaye ameamua kurejea nchini England baada ya kudumu China kwa miaka miwili tu na kuondoka kama mchezaji huru mwezi Novemba 2018.
Awali ziliripotiwa taarifa kuwa kiungo huyo ameshindwa kuishi China kutokana na kuwa mbali na familia yake ambayo imeweka makazi nchini England licha ya John Obi Mikeli kuondoka katika taifa hilo, hivyo ameamua kurudi kukaa na familia yake.
Obi amerudi Uingereza na sasa ameamua kujiunga kwa mkataba wa muda mfupi akiwa kama mchezaji huru katika klabu ya Middlesbrough inayosaka tiketi ya kurejea Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2019/20.
Obi ambaye ameondoka Chelsea mwaka 2017 baada ya kudumu kwa miaka 11, ameshinda mataji mbalimbali akiwa na Chelsea kama Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Ulaya na FA.