Mchezaji anyimwa jezi namba 9 AC Milan
Timu ya AC Milan ya nchini Italia imekataa kumpa jezi namba 9 mshambuliaji wao mpya kutokea Genoa waliyomsajili kwa dau la pauni milioni 30 Krzysztof Piatek.
Uongozo wa AC Milan umekataa kumpa nyota huyo jezi namba 9 kama alivyoomba na kumtaka aoneshe uwezo kwanza kabla ya kupewa jezi namba hiyo iliyofanyiwa makubwa na kina Inzaghi.
Awali kabla ya wachezaji kadhaa kuwahi kuivaa jezi hiyo iliwahi kuvaliwa na wachezaji mahiri kama Jose Altafini, Marco van Basten na Filippo Inzaghi
Mpoland huyo ameomba kuvaa jezi hiyo iliyokuwa imeachwa wazi na Gonzalo Higuan aliyeamua kusitisha mkataba wake wa mkopo na kujiunga na Chelsea anapaswa kuonesha uwezo kwanza ndio apewe.
Krzysztof Piatek mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na AC Milan akisaini mkataba utakoisha mwaka 2023 .
Nyota huyo mpya ambaye ameingia AC Milan amepewa jezi namba 19 kwanza, licha ya kung’aa kwake kwa muda mfupi zaidi akiwa na Genoa tu ndani ya miezi sita akifunga goli 19 ndani ya mechi 21, anahitaji kufanya makubwa zaidi ya kuwaridhisha viongozi wampe jezi namba 9.