Monaco yamsimamisha kazi Thierry Henry
AS Monaco imemsimamisha kazi kocha wake Thierry Henry kutokana na timu hiyo kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya unaowafanya kuwepo katika eneo la kushuka daraja katika Ligue 1
Timu hiyo haijashinda mchezo wowote wa ligi tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana walipoifunga Amiens bao 2-0.
Taarifa hiyo ya kusimamishwa imekuja siku mbili baada ya kutolewa katika French Cup na Metz.
Baada ya kuadhibiwa na Strasbourg kwa goli 5-1 jumamosi iliyopita,Monaco inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligue 1
Henry ameichukua Monaco miezi mitatu iliyopita na tangu achukue kazi hiyo timu hiyo imezidi kufanya vibaya.
Taarifa ya klabu inasema kuwa, wamesimamisha kazi Thierry Henry wakati wakiwa wanasubiri maamuzi ya mwisho kuhusu mustakabali wake.