Polisi watangaza kuhitimisha msako wa Emiliano Sala
Mamlaka ya polisi ya Guernsey iliyokuwa inahusika na kutafuta ndege iliyopotea na mshambuliaji wa Cardiff Emiliano Sala imetangaza kufikia tamati ya msako huo.
Kazi hiyo ya kumtafuta mchezaji huyo na rubani ulianza tangu jumatatu jioni ndege hiyo ilipopotea na kufikia tamati leo alhamisi mchana bila mafanikio yoyote.
Taarifa kutoka kwa Captain David Barker iliyotolewa na mamlaka ya polisi Guernsey, inasema kuwa licha ya jitihada zao za takribani saa 80, wakitumia ndege tatu, helikopta tano, boti mbili vilevile na msaada kutoka meli zinazopita na boti za wavuvi, hawajafanikiwa kupata hata kiashiria chochote cha ndege hiyo, rubani au abiria (Sala). Sala,28, ambaye ni Muargentina alisajiliwa na Cardiff jumamosi iliyopita kwa ada ya usajili wa klabu hiyo pauni milioni 15 akitokea Nantes ya nchini France.
Baada ya kusaini mkataba wake na Cardiff alirejea nchini France kuwaaga wachezaji aliokuwa anacheza nao Nantes na siku ya jumatatu akapanda ndege binafsi kurejea Wales tayari kuanza kazi na ndipo ndege hiyo ilipopotea baada ya kupoteza mawasiliano