Hazard si kiongozi mzuri,asema Sarri
Kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri ambaye hivi leo ameungana na mshambuliaji wake aliyekuwa anamfundisha katika klabu ya Napoli Gonzalo Higuan kwa mkopo wa miezi sita akitokea Juventus ya nchini Italia, kocha huyo amemzungumzia nyota wake raia wa Ubelgiji Eden Hazard kuwa ni mchezaji mkubwa duniani.
Maurizio Sarri ambaye pamoja na kumsifia kwa kueleza sifa za mchezaji wake Eden Hazard kuwa ni aina ya mchezaji wenye uwezo wa kuipa timu matokeo ndani ya dakika moja au mbili uwanjani.
Ameeleza kuwa mchezaji huyo ni mzuri kama yeye lakini sio kama kiongozi uwanjani.
.
“Sijui , lakini kwa hivi sasa ni mchezaji mzuri yeye binafsi lakini sio kama kiongozi, ni mtu muhimu kwetu kwa sababu ni mchezaji mzuri. Siku zote amekuwa na uwezo wa kushinda mechi ndani ya dakika 2 au wakati mwingine hata dakika moja lakini wakati huo huo sio kiongozi mzuri ila ni mchezaji mzuri, ni moja kati ya wachezaji bora duniani ila sio kiongozi mzuri” alisema Sarri baada ya kuulizwa mchango wa mchezaji huyo uwanjani kama kiongozi.