Neymar kuwakosa Man United
PSG ameingia katika wasiwasi ya kumkosa nyota wake Neymar Jr katika mchezo wao wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Man United kufuatia mchezaji huyo kuumia katika kifundo cha mguu wake wa kulia kwenye mchezo wa jana wa French Cup dhidi ya Strasbourg.
Mchezaji huyo alitoka uwanjani akiwa na machozi baada ya kupata maumivu hayo katika sehemu ile ile aliyoumia msimu uliopita na kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kocha wa PSG Thomas Tuchel alikuwa mkali akidai kuwa mwamuzi ameshindwa kumlinda mchezaji wake mpaka kusababibisha kuumia.
Hata hivyo kocha wa Strasbourg Thierry Laurey amesema aina ya uchezaji wa Neymar wa kutoheshimu wapizani ndio unasababisha kufanyiwa madhambi.
“ Ni aina yake ya uchezaji. Kama unacheza kama vile usilalamike kama utachezewa rafu “ alisema kiungo wa Strasbourg Anthony Goncalves.
‘ Ni mchezaji mkubwa, na nina-muheshimu kama mchezaji , lakini sisi hatupo hapa ili kumfurahisha . Sisi hatupo hapa ili kumfanya aonekane mzuri ‘
Tuchel sasa anasubiri kujua ni kwa muda gani atamkosa nyota huyo.
PSG wataivaa Man United katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 Bora Februari 12 Old Trafford na tayari wapo katika hatihati ya kumkosa kiungo wao Marco Verratti ambaye aliumia katika kifundo cha mguu wake wikiendi iliyopita.