Bifu na Vieira lamng’oa Balotelli Nice
Mshambuliaji wa zamani wa timu za Liverpool na Manchester City Mario Balotelli ameachwa kujiunga bure na klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa baada ya klabu yake ya Nice ya Ufaransa pia kuamua kumuacha ondoke huru kutokana na kutokuwa katika mahusiano mazuri na kocha wa timu hiyo Patrick Vieira.
Balotelli mwenye umri wa miaka 28 anadaiwa kuachwa kama mchezaji huru na timu yake ya Nice ambayo licha ya kujiunga nayo ikiwa na msimu mbaya akitokea Liverpool mwaka 2016 aliifanyia makubwa kwa kuifungia mabao muhimu yaliyopelekea kuiwezesha klabu hiyo kuvuna alama muhimu katika michezo yake ya Ligue 1.
Hata hivyo Sky Sports Italia imeripoti kuwa Mario Balotelli atavuna pauni milioni 2.7 atakopoichezea Marseille katika michezo 17, Balotelli alikuwa na misimu miwili mizuri akiwa na Nice kwa kuifungia jumla ya mabao 33 katika misimu yote ila mahusiano yake mabovu na kocha Patrick Vieira ndio yamepelekea kuachwa kwake.