Naomi Osaka atinga fainali nyingine Grand Slam
Wengi walimfahamu kupitia katika fainali ya US Open mwaka jana, ambapo alimfunga Idol wake Serena Williams na kuchukua Grand Slam yake ya kwanza
Safari hii Idol wake huyo hajafika hata hatua ya nusu fainali katika michuano ya Australian Open inayoendelea huko Australia, ila yeye amefika hatua ya fainali.
Si mwingine, ni mwanadada Naomi Osaka. Anafika katika fainali mbili mfululizo za Grand Slam.
Mjapan huyu,21, amefika hatua hiyo baada ya kumfunga mwanadada Karolina Pliskova kwa seti 6-2 4-6 6-4 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwa saa moja na dakika 53.
Amekuwa Mjapan wa kwanza kufika fainali ya Australian Open katika Open Era.
Naomi sasa katika mchezo wa fainali jumamosi hii atakutana na Petra Kvitova kutoka Czech ambaye amefika hatua hiyo kwa kumfunga Mmarekani Danielle Collins 7-6,6-0.